• HABARI MPYA

  Thursday, April 20, 2023

  MAN CITY NA REAL, AC NA INTER MILÁN NUSU FAINALI


  TIMU ya Manchester City imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya sare ya 1-1 na wenyeji, Bayern Munich usiku wa Jumatano Uwanja wa Allianz Arena Munich.
  Bao la Man City lilifungwa na Erling Haaland dakika ya 57, kabla ya Joshua Kimmich kuisawazishia Bayern Munich dakika ya 83.
  Manchester City inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya kuichapa Bayern Munich 3-0 kwenye mechi ya kwanza England na sasa itakutana na mabingwa watetezi, Real Madrid.
  Real Madrid wataanzia nyumbani Mei 9 kabla ya kwenda Etihad kwa mchezo wa marudiano Mei 16. Mechi nyingine ya marudiano ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Inter Milán imelazimishwa sare ya 3-3 na Benfica Italia. 
  Inter inakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 5-3 baada ya kuichapa Benfica 2-0 Ureno na sasa watakutana na AC Milan katika Milán Derby mechi zote mbili zikipigwa San Siro, au Giuseppe Meazza Mei 9 na Mei 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY NA REAL, AC NA INTER MILÁN NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top