• HABARI MPYA

  Thursday, April 27, 2023

  MASHABIKI WAZOMEA WACHEZAJI BAADA YA KIPIGO CHA BRENTFORD


  MASHABIKI wenye hasira wa Chelsea waliwazomea wachezaji baada ya kichapo cha 2-0 nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London mbele ya Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano.
  Mabao ya Brentford yamefungwa na Cesar Azpilicueta dakika ya 37 na Bryan Mbeumo dakika ya 78 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 47 katika mchezo wa 33 na kusogea nafasi ya tisa.
  Kwa Kocha Frank Lampard huo ni mchezo wa tano mfululizo anafungwa tangu arejee kazini Chelsea na timu inabaki na pointi zake 39 za mechi 32 sasa ikihamia nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHABIKI WAZOMEA WACHEZAJI BAADA YA KIPIGO CHA BRENTFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top