• HABARI MPYA

  Saturday, April 29, 2023

  MAYELE APEWA JEZI YA HESHIMA YA MABAO 50 YANGA


  WACHEZAJI wa Yanga SC leo wamemkabidhi mwenzao, mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele jezi ya idadi ya mabao aliyofunga hadi sasa, 50 zoezi ambalo limefanyika kambini kwao Uwanja wa Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Na imekuwa siku moja kabla ya mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria kesho Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo utakaoanza Saa 2:00 usiku Yanga inahitaji hata sare ili kwenda Nusu Fainali baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Nigeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APEWA JEZI YA HESHIMA YA MABAO 50 YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top