• HABARI MPYA

  Tuesday, April 18, 2023

  HATIMA YA AISHI MANULA KUJULIKANA LEO SIMBA SC


  KIPA namba moja wa Simba, Aishi Salum Manula leo atakutana na jopo la matabibu wa timu kutazamwa hali yake ili kujua kama yuko tayari kuanza mazoezi kuelekea mchezo dhidi ya Wydad Casablanca.
  Simba watamenyana na Wydad Casablanca Jumamosi katika mechi ya kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Aishi alikosekana kwenye mechi mbili zilizopita za Ligi Kuu ya nyumbani dhidi ya Ihefu huko Mbarali Aprili 10 na Yanga jana, baada ya kuumia kwenye Azam Sports Federation Cup Aprili 7 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Lakini Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kikosi kinaanza mazoezi leo Uwanja wa Mo Simba Arena baada ya mapumziko ya siku moja ya jana kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya mtani, Yanga kwenye Ligi Kuu Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kipa namba mbili pia, Beno Kakolanya anatarajiwa kuwa tayari kwa mechi hizo mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika, ukwemo na ule Aprili 28 Casablanca baada ya yeye pia kukosekana kwenye mechi zote mbili hizo zilizopita kwa sababu ya majeruhi pia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HATIMA YA AISHI MANULA KUJULIKANA LEO SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top