• HABARI MPYA

  Sunday, April 30, 2023

  NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA NI AL AHLY V ESPERANCE NA MAMELODI V WYDAD


  VIGOGO wa Afrika, Al Ahly wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Raja Club Athletic jana Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablaca nchini Morocco.
  Matokeo hayo yanawafanya waende Nusu Fainali baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza, nyumbani nchini Misri na watakutana na Esperance ya Tunisia ambayo imeitoa JS Kabylie ya Algeria.
  Nyota Mualgeria, Yousri Bouzouk aliinyima nafasi ya kufunga Al Ahly dakika ya 45 baada ya kupiga nje penalti kufuatia yeye mwenyewe kuangushwa na kiungo wa Kimataifa wa Mali, Aliou Dieng.
  Na ilikuwa nafasi ya pili Yousri Bouzouk anapoteza baada ya dakika ya 28 kupata mpira akiwa eneo zuri la kufunga, lakini shuti lake likaokolewa na kipa Mohamed Elshenawy.
  Esparence ilishinda 1-0 mechi ya kwanza Algeria wiki iliyopita kabla ya jana kulazimisha sare ya 1-1 Tunis.
  Mechi nyingine za marudiano za Robo Fainali, wenyeji Mamelodi Sundowns wameitoa Belouizdad baada ya kuichapa 2-1 jana Afrika Kusini na kufanya ushindi wa jumla wa 6-2 kufuatia kushinda 4-1 kwenye mchezo wa kwanza Algeria.
  Mamelodi watakutana na mabingwa watetezi, Wydad Club Athletic ya Morocco imeitoa Simba SC ya Tanzania kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya 1-1 kila timu ikishinda 1-0 kwake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA NI AL AHLY V ESPERANCE NA MAMELODI V WYDAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top