• HABARI MPYA

  Saturday, April 15, 2023

  JOB AONGEZA MKATABA WA KUENDELEA NA MAJUKUMU YANGA


  BEKI anayecheza pembeni na katikati, Dickson Nickson Job ‘Mamba’ (22) ameongeza mkataba wa kuendelea kuichezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
  Taarifa ya Yanga jioni hii imesema Job ameongeza mkataba, ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wa watani wa jadi, dhidi ya Simba kesho Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Job aliyejiunga na Yanga mwaka 2021 kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, alikuwa anahusishwa na wapinzani wakuu wa klabu yake katika vita ya mataji, Azam na Simba.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOB AONGEZA MKATABA WA KUENDELEA NA MAJUKUMU YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top