• HABARI MPYA

  Thursday, April 13, 2023

  WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATAKA NETIBOLI IFUFULIWE


  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameagiza kufufuliwa kwa mchezo wa Netiboli nchini.
  Akizungumza Bungeni Jijini Dodoma leo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Netiboli ipewe kipaumbele na ianze kufanyika kwa kuwa ni miongoni mwa michezo iliyokua inafanya vizuri ndani na nje ya nchi.
  Waziri Majaliwa pia ameipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Kuratibu vyema mashindano mbalimbali yanayofanyika ndani na nje ya nchi ambayo yameendelea kuitangaza vyema Tanzania.
  Majaliwa ametoa rai kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI zihakikishe kuwa Sekta ya michezo inaendelea kupewa kipaumbele katika ngazi zote hapa nchini.
  Majaliwa ametoa pongezi na rai hiyo  leo Aprili 13, 2023 Bungeni jijini Dodoma alipokutana na Mabingwa wa Soka  Afrika kwa upande wa Shule za Sekondari, timu ya Fountain Gate waliofika Bungeni jijini Dodoma kupongezwa kwa kutwaa Ubingwa huo.
  "Naupongeza Uongozi wa Shule hii pamoja na Alliance ya jijini Mwanza kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuunga mkono maendeleo ya Sekta ya Michezo nchini, tunawashukuru sana naamini mtaendelea kufanya hivyo katika michezo mingine" Amesisitiza Mhe. Majaliwa.
  Ametumia nafasi hiyo kuipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuendelea kufanya vizuri katika maendeleo ya Sekta zake, ambapo pia amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa kufanya mabadiliko katika Shirikisho hilo ambalo sasa mafanikio ya mchezo wa Soka yanaonekana.
  Aidha, ameagiza Wizara ya Elimu, TAMISEMI na Wizara ya Utamaduni kuhakikisha somo la michezo linafundishwa shuleni kwa kuwa waalimu wa somo hilo wapo katika chuo cha Malya na Butimba.
  Awali, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara itaendelea kuratibu mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA kwa kuwa ni miongoni mwa mashindano yanayozalisha wachezaji wengi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATAKA NETIBOLI IFUFULIWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top