• HABARI MPYA

  Sunday, April 30, 2023

  WENYE TAJI LAO MAN CITY YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Fulham leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na washambuliaji Mnorway, Erling Haaland kwa penalti dakika ya tatu na Muargentina Julian Álvarez dakika ya 36, wakati la Fulham limefungwa na Carlos Vinícius dakika ya 15.
  Kwa ushindi huo, Manchester City imefikisha pointi 76 katika mchezo wa 32 na kurejea juu ya msimamo wakiizidi pointi moja Arsenal ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, huku Fulham ikibaki na pointi zake 45 za mechi 33 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENYE TAJI LAO MAN CITY YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top