// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BILIONEA MO DEWJI AWEKA BAYANA: “NINA IMANI NA SALUM TRY AGAIN SIMBA” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BILIONEA MO DEWJI AWEKA BAYANA: “NINA IMANI NA SALUM TRY AGAIN SIMBA” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, April 19, 2023

  BILIONEA MO DEWJI AWEKA BAYANA: “NINA IMANI NA SALUM TRY AGAIN SIMBA”


  RAIS wa heshima wa Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji amemsifu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salum Abdallah Muhene ‘Try Again’ kwa kazi nzuri anayoifanya na kusema kwamba Ana imani naye.
  Sifa hizo zinakuja baada ya Simba SC kuifunga Yanga 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Jumapili Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Simba pia imefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Jumamosi itamenyana na mabingwa watetezi, Wydad Casablanca.
  Robo Fainali hiyo ya kwanza itafanyika Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 28 Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
  Tayari Simba ipo katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) ambako itamenyana na Azam FC mwishoni mwa mwezi huu.
  Simba yenye pointi 63, inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikizidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BILIONEA MO DEWJI AWEKA BAYANA: “NINA IMANI NA SALUM TRY AGAIN SIMBA” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top