• HABARI MPYA

  Saturday, April 29, 2023

  NABI ASEMA DHAMIRA YA YANGA NI KUWAFUNGA TENA RIVERS


  KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Nasredeen Nabi amesema dhamira yao ni kushinda mchezo wa kesho wa marudiano Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo huo wa kesho Nabi amesema ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza hautakuwa na maana kama kesho hawatashinda.
  Mechi ya kwanza Yanga ilishinda 2-0, mabao ya mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele Uwanja wa Venue Godswill Akpabio International mjini Uyo, Nigeria Jumapili iliyopita.
  Ikumbukwe mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambazo mechi ya kwanza zilitoka sare ya 1-1 Misri Jumapili iliyopita.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NABI ASEMA DHAMIRA YA YANGA NI KUWAFUNGA TENA RIVERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top