• HABARI MPYA

  Saturday, April 29, 2023

  JKT, KITAYOSCE NA PAMBA ZOTE ZATOA SARE CHAMPIONSHIP


  TIMU za JKT Tanzania, Kitayosce na Pamba FC zote zimetoa sare katika mechi zao za leo za Ligi ya Championship na kufanya msimamo uendelee kusomeka kama ulivyokuwa.
  JKT Tanzania imefungana mabao 3-3 na Mashujaa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo huko Mbweni, Dar es Salaam, Pamba imefungana bao 1-1 na African Sports Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na Kitayosce haijafungana na Fountain Gate Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
  Msimamo wa Championship sasa JKT Tanzania ambayo tayari imekwishapanda Ligi Kuu ina pointi 63 za mechi 27, Kitayosce 54 na Pamba FC 53 baada ya wote kucheza mechi 26.
  Mechi nyingine ya Championship leo Mbeya Kwanza imeichapa Pan Africans 2-1 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
  Mbeya Kwanza imefikisha pointi 37 na kusogea nafasi ya saba na Pan Africans sasa ina pointi 24 na kusogea nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT, KITAYOSCE NA PAMBA ZOTE ZATOA SARE CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top