• HABARI MPYA

  Wednesday, April 26, 2023

  SIMBA SC WAWASILI SALAMA CASABLANCA KWA SHUGHULI YA IJUMAA


  KIKOSI cha Simba SC kimewasili salama Jijini Casablanca nchini Morocco usiku huu kwa ajili ya mchezo wa marudiano na wenyeji, Wydad Club Athletic Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ijumaa Uwanja wa Mohamed V.
  Simba inahitaji sare kwenda Nusu Fainali baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa hao watetezi Jumamosi, bao pekee la mshambuliaji Mkongo, Jean Othos Baleke dakika ya 30 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Wakati Wydad ina mataji matatu ya CAF Champions League (1992, 2017 na 2021–22), mafaniko makubwa kwa Simba kwenye michuano hiyo ni kufika Nusu Fainali mwaka 1974 ilipoitoa Hearst Of Oak ya Ghana kwa mabao 2-1 kabla ya kutolewa na Ghazl El Mahalla yenye maskani yake mji wa El Mahalla El Kubra kwa penalti 3-0 kufuatia sare ya jumla ya 1-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC WAWASILI SALAMA CASABLANCA KWA SHUGHULI YA IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top