• HABARI MPYA

  Friday, April 21, 2023

  BALOZI WA MOROCCO AFUTURU NA WACHEZAJI WYDAD CASABLANCA DAR


  BALOZI wa Morocco nchini Tanzania, Zakaria El Koumiri jana aliwaalika na kufuturu nao wachezaji wa klabu ya Wydad AC kuelekea mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba SC kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Japokuwa mechi itaanza Saa 10:00 jioni, lakini tangu wamewasili  hapa Jumatano Wydad wamekuwa wakifanya mazoezi usiku tu Uwanja wa Gymkhana ingawa kwa mujibu wa kanuni leo watafanya mazoezi Saa 10:00 Uwanja wa Benjamín Mkapa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALOZI WA MOROCCO AFUTURU NA WACHEZAJI WYDAD CASABLANCA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top