• HABARI MPYA

  Friday, April 21, 2023

  ROBERTINHO AWAONYA WYDAD WASIICHUKULIE POA SIMBA SC


  KOCHA Mbrazil wa Simba SC, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo 'Robertinho' amewaonya mabingwa wa Afrika, Wydad Athletic Club kuelekea mechi baina yao kesho.
  Simba watakuwa wenyeji wa Wydad Casablanca kesho Saa 10:00 jioni katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 28 Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco. 
  Kihistoria Simba na Wydad zimekutana mara moja tu Mei 28, mwaka 2011 mjini Cairo nchini Misri katika mchezo wa mchujo wa mkondo mmoja kuwania kuingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na Wydad iliibuka na ushindi wa 3-0.
  Mchezo huo ulifuatia timu zote hizo kutolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika Raundi ya Kwanza na ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini Simba walimkatia Rufaa beki Janvier Besala Bokungu kwamba hakuwa mchezaji halali wa timu hiyo ya DRC.
  Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likajiridhisha Mazembe ilitumia mchezaji kimakosa na ndipo ikaitisha mechi ya Simba na Wydad Cairo Mei 28, mwaka 2011 na kuiondoa mashindanoni timu ya DRC.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROBERTINHO AWAONYA WYDAD WASIICHUKULIE POA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top