• HABARI MPYA

  Wednesday, April 19, 2023

  REAL MADRID NA AC MILAN ZATANGULIA NUSU FAINALI


  WENYEJI, Chelsea wametupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kichapo cha mabao 2-0 mbele ya mabingwa watetezi, Real Madrid usiku wa Jumanne Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Real Madrid yamefungwa na kinda wa miaka 22, Mbrazil Rodrygo Silva de Goes yote mawili dakika ya 58 na 80.
  Kwa matokeo hayo, Real Madrid wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-0 baada ya kuwachapa Chelsea 2-0 pia Madrid wiki iliyopita.
  Katika Nusu Fainali Real itakutana na mshindi wa jumla katí ya Manchester City na Bayern Munich zinazomenyana leo katika mchezo wa marudiano Ujerumani. Mechi ya kwanza Man City ilishinda 3-0 England.
  Mchezo mwingine wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa, Napoli imelazimishwa sare ya 1-1 na AC Milan ambao wanakwenda Nusu Fainali kwa ushindi wa 2-0 baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza.
  AC Milan watakutana na mshindi wa jumla latí ya Benfica na Inter Milan zinazorudiana leo Milan. Mechi ha kwanza Inter walishinda 2-0 Ureno.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID NA AC MILAN ZATANGULIA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top