• HABARI MPYA

  Tuesday, April 18, 2023

  YANGA SC KUONDOKA ALHAMISI KUIFUATA RIVERS NIGERIA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wanatarajiwa kuondoka nchini Alhamisi ALfajiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Rivers United Jumapili Uwanja wa Godswill Akpabio International mjini Uyo huko Akwa Ibom Kusini mwa Nigeria.
  Yanga inahitaji kwenda kukaza ili kuja kumaliza vizuri kwenye mechi ya nyumbani Aprili 30, waweze kulipa kisasi cha kutolewa na Rivers katika Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa msimu uliopita kwa vichapo vya 1-0 nyumbani na ugenini. 


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC KUONDOKA ALHAMISI KUIFUATA RIVERS NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top