• HABARI MPYA

  Saturday, April 22, 2023

  SIMBA SC YAWAZIMA MABINGWA WA AFRIKA, WYDAD YAFA 1-0 DAR


  WENYEJI, Simba SC wametanguliza mguu mmoja katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Wydad Athletics Club leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mkongo, Jean Othos Baleke dakika ya 30 akimalizia shuti la Kibu Dennis Prosper kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Mzambia, Clatous Chama.
  Sasa Simba itahitaji kwenda kuulinda ushindi huo mwembamba kwenye mchezo wa marudiano Aprili 28, Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco ili kwenda Nusu Fainali ya pili tu kihistoria ya michuano hiyo mikubwa ya klabu barani tangu mwaka 1974 ilipoitoa Hearst Of Oak ya Ghana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWAZIMA MABINGWA WA AFRIKA, WYDAD YAFA 1-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top