• HABARI MPYA

  Saturday, April 22, 2023

  DIOGO JOTA APIGA MBILI LIVERPOOL YASHINDA 3-2


  WENYEJI, Liverpool FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield, Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota mawili, dakika ya 47 na 55 na Mohamed Salah dakika ya 70, wakati ya Nottingham Forest yamefungwa na Neco Williams dakika ya 51 na Morgan Gibbs-White dakika ya 67.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 31 na kusogea nafasi ya saba, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake 27 za mechi 32 nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DIOGO JOTA APIGA MBILI LIVERPOOL YASHINDA 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top