• HABARI MPYA

  Monday, April 17, 2023

  SERIKALI YAMPONGEZA MWANARIADHA WA TANZANIA KUNG’ARA MAREKANI


  WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Hadhara Chana amempongeza Mwanariadha, Gabriel Geay kwa kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon nchini Marekani.
  Geay amemaliza akitumia muda wa Saa 2:06:04, nyuma ya Mkenya, Evans Chebet aliyetumia muda wa Saa 2:05:54, nafasi ya tatu na ya nne imekwenda kwa Wakenya pia, Benson Kipruto (2:06:06) na Albert Korir (02:08:01), wakati Mmorocco Zouhair Talbi ameshika nafasi ya tano akitumia Saa 2:08:35.
  Ndoto za mshikilia rekodi ya Dunia, Mkenya mwingine, Eliud Kipchoge kushinda Marathoni ya 16 kati ya 18 alizoshiriki ziligonga mwamba baada ya kuambulia nafasi ya sita akitumia muda wa Saa 2:09:23.
  Wakati huo huo: Waziri Pindi Chana pia amempongeza mwanariadha mwingine wa mbio ndefu, Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya tatu katika mbio za Yangzhou Jianzhen International Half Marathon zilizofanyika jana China.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERIKALI YAMPONGEZA MWANARIADHA WA TANZANIA KUNG’ARA MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top