• HABARI MPYA

    Tuesday, April 25, 2023

    AZAM FC YAUNGANA NA SERIKALI KUPIGA VITA UKATILI WA KIJINSIA


    KLABU ya Azam FC imeungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika kupiga vita ukatili wa kijinsia na watoto.
    Katika kuliwekea uzito jambo hilo, Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, alikutana na viongozi wa Azam FC, 
    Makamu Mwenyekiti, Omary Kuwe na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat' kujadili kwa kina watakavyoshirikiana kupinga ukatili huo.
    Wizara hiyo, ipo katika kampeni kubwa ya kutokomeza ukatili huo, ambapo imeandaa Tamasha kubwa la Zijue Fursa, Imarisha Uchumi, Kataa Ukatili (ZIFIUKUKI) litakalofanyika kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam kuanzia Ijumaa Aprili 27 hadi 29 mwaka huu.
    Dkt. Gwajima, amesema kuwa mbali na tamasha hilo kushirkisha michezo, pia litakuwa na fursa mbalimbali za uwezeshaji kiuchumi katika jamii, kama ilivyo sera ya Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
    Alisema, "Tamasha hili limebeba taswira nzima ya kampeni ya serikali kupitia Wizara wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum iliyozinduliwa mwaka 2017-2018 inayosema twende pamoja, Tanzania sasa, Ukatili basi."
    Naye Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', aliishukuru Serikali kwa kuwachagua kuwa miongoni mwa mabalozi wake katika kampeni hiyo na kuahidi kuwa watashiriki kikamilifu kupinga ukatili wa kijinsia na watoto.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAUNGANA NA SERIKALI KUPIGA VITA UKATILI WA KIJINSIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top