• HABARI MPYA

  Thursday, April 27, 2023

  WAZIRI WA MICHEZO AWAZAWADIA MAMILIONI WANARIADHA GEAY NA SIMBU


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (kulia) akimkabidhi zawadi ya Shilingi Milioni 3 Mwanariadha wa Kimataifa Gabriel Geay ambaye ameshika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Riadha (Buston Marathon) yaliyofanyika hivi  karibuni nchini Marekani. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Hamis Mwinjuma. Fedha hizo zimetolewa na Wizara ya  Utamaduni, Sanaa na Michezo.


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akimkabidhi zawadi ya Shilingi Milioni 2 iliyotolewa na wizara hiyo, kwa  Mwanariadha wa Kimataifa Aliphonce Simbu (katikati)  ambaye ameshika nafasi ya tatu katika mbio za Yangzhou Jianzhen International Half Marathon. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma. Tukio hilo limefanyika leo Aprili 27, 2023 jijini Dodoma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI WA MICHEZO AWAZAWADIA MAMILIONI WANARIADHA GEAY NA SIMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top