• HABARI MPYA

  Sunday, April 23, 2023

  TWAHA KIDUKU AMSHINDA BONDIA WA GEORGIA KWA POINTI

  BONDIA Twaha Kassim Rubaha 'Twaha Kiduku' usiku wa jana amefanikiwa kutetea taji lake la Mabara la UBO baada ya kumchapa kwa kumshinda kwa pointi Iago Kiziria wa Georgia katika pambano lililofanyika ukumbi wa Tanzania Hall mjini Morogoro.
  Ushindi huo unamfanya pia Kiduku abebe na taji la Shirikisho la Masumbwi Tanzania (PST) lililoachwa wazi na Suleiman Kidunda kwa kushindwa kulitetea kwa muda mrefu.
  Pambano lingine, majaji walizomewa na mamia waliojitokeza ukumbi wa Tanzania Hall baada ya kumpa ushindi wa pointi Juma Choky dhidi ya Loren Japhet, wote wa Dar es Salaam.
  Baada ya pambano hilo, Loren alilalamika imekuwa kawaida kwake kudhulumiwa ushindi akipigana nyumbani na kwa sababu hiyo hatapigana nchini, huku Choky akifurahia matokeo hayo.  

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWAHA KIDUKU AMSHINDA BONDIA WA GEORGIA KWA POINTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top