• HABARI MPYA

  Tuesday, April 18, 2023

  MAMA SAMIA AMWAGIA PONGEZI MWANARIADHA ALIYESHINDA MAREKANI


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha, Gabriel Geay kwa kushika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon nchini Marekani.
  "Nakupongeza Gabriel Gerald Geay kwa kuwa mshindi wa pili katika Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya Boston yaliyofanyika leo nchini Marekani. Jitihada zako zimeijengea heshima Tanzania. Nakutakia kheri katika kusonga mbele zaidi. Serikali itaendelea kuwaunga mkono wanamichezo," amesema Rais Samia. 
  Ndoto za mshikilia rekodi ya Dunia, Mkenya mwingine, Eliud Kipchoge kushinda Marathoni ya 16 kati ya 18 alizoshiriki ziligonga mwamba baada ya kuambulia nafasi ya sita akitumia muda wa Saa 2:09:23.
  Wakati huo huo: Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Hadhara Chana pamoja na kumpongeza Geay, pia amempongeza mwanariadha mwingine wa mbio ndefu, Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya tatu katika mbio za Yangzhou Jianzhen International Half Marathon zilizofanyika jana China.
  Geay amemaliza akitumia muda wa Saa 2:06:04, nyuma ya Mkenya, Evans Chebet aliyetumia muda wa Saa 2:05:54, nafasi ya tatu na ya nne imekwenda kwa Wakenya pia, Benson Kipruto (2:06:06) na Albert Korir (02:08:01), wakati Mmorocco Zouhair Talbi ameshika nafasi ya tano akitumia Saa 2:08:35.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMA SAMIA AMWAGIA PONGEZI MWANARIADHA ALIYESHINDA MAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top