• HABARI MPYA

  Sunday, April 30, 2023

  YANGA SC WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO


  HATIMAYE Yanga SC imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya sare ya bila kufungana na Rivers United ya Nigeria usiku huu katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Yanga wanakwenda Nusu Fainali kwa faida ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita Nigeria, mabao ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele.
  Yanga sasa itamenyana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambayo imeitoa Pyramids ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1, ikitoa sare ya 1-1 Cairo wiki iliyopita na kushinda 1-0 leo Phokeng, NW.
  Mechi ya kwanza Yanga na Marumo Gallants itafanyika Dar es Salaam Mei 10 na marudiano yatafuatia Afrika Kusini Mei 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top