• HABARI MPYA

  Sunday, April 16, 2023

  CHELSEA HALI BADO TETE, YAPIGWA TENA DARAJANI


  WENYEJI, Chelsea mambo yamezidi kuwaendea kombo licha ya mabadiliko ya benchi la Ufundi baada ya jana pia kuchapwa 2-1 na Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Brighton yamefungwa na Danny Welbeck dakika ya 42 na Julio Enciso dakika ya 69 baada ya Chelsea kutangulia na bao la Conor Gallagher dakika ya 13.
  Kwa ushindi huo, Brighton inafikisha pointi 49 katika mchezo wa 29 ingawa inabaki nafasi ya saba na Chelsea inabaki na pointi zake 39 za mechi 31 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA HALI BADO TETE, YAPIGWA TENA DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top