• HABARI MPYA

  Saturday, April 22, 2023

  MAN CITY YATINGA FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND


  TIMU ya Manchester City imeibuka na mabao 3-0 dhidi ya Sheffield United FC katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la FA England leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Mabao yote ya Manchester City leo yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez la kwanza kwa penalti dakika ya 43 na mengine dakika ya 61 na 66 akimalizia kazi nzuri ya kungo wa Kimataifa wa England, Jack Grealish.
  Sasa Manchester City itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya Brighton & Hove Albion na Manchester United katika Fainali ya FA itakayopigwa Juni 3 hapo hapo Wembley.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YATINGA FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top