• HABARI MPYA

  Sunday, April 16, 2023

  BUKAYO SAKA AKOSA PENALTI ARSENAL YATOA SARE


  TIMU ya Arsenal imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji, West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Jesus dakika ya saba na Martin Ødegaard dakika ya 10, wakati ya West Ham United yamefungwa na Mohamed Benrahma kwa penalti dakika ya 33 na Jarrod Bowen dakika ya 54.
  Bukayo Saka aliikosesha Arsenal bao baada ya kukosa penalti dakika ya 52 na kwa matokeo hayo wanafikisha pointi 74 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao, West Ham United wanafikisha pointi 31 za mechi 30, ingawa wanabaki nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BUKAYO SAKA AKOSA PENALTI ARSENAL YATOA SARE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top