• HABARI MPYA

  Monday, April 17, 2023

  AISHI MANULA AMWAGIA PONGEZI ALLY SALIM KWA KAZ YA JANA


  KIPA namba moja wa Simba, Aishi Salum Manula amempongeza kipa wa tatu, Ally Salim Juma kwa kudaka vizuri jana na kuiwezesha timu kushinda 2-0 dhidi ya watani wa jadi, Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Aishi aliandika jana kwenye ukurasa wake wa Instagram; "No Manula, No Beno Kakolanya, No problem Ally Salim Juma,". 
  Naye Ally akapost; "Kwanza kabisa namshukuru mwenyezi Mungu kwa kunijaalia Clean Sheet ya pili, nawashukuru makipa wenzangu Beno na Aishi kwa kunijenga zaidi na pia nawashukuru benchi la ufundi kunipa nafasi," amesema.
  Kipa huyo huyo wa tatu  akaongeza kwamba anawashukuru sana pia mashabiki wa Simba kwa upendo wao kwake.
  Kocha wa Simba, Mbrazil Robert Oliveira alilazimika kumuanzisha Ally Salum katika mechi ngumu dhidi ya Yanga kwa sababu makipa wote wawili wakubwa, Aishi na Benno Kakolanya walikuwa majeruhi.
  Chipukizi huyo aliyepandishwa kutoka timu ya vijana akaenda kusimama vyema langoni na kuisaidia timu kubeba pointi tatu, akikikumbushia Oktoba 18, mwaka 2014 Simba ilipolazimika kumuanzisha kipa mwingine wa tatu, Peter Manyika katika mechi ya Simba.
  Kama ilivyokuwa jana, Oktoba 18, mwaka 2014 makipa wote wakubwa walikuwa wagonjwa, Ivo Mapunda na Hussein Sharrif 'Cassilas', hivyo ikabidi Manyika ambaye naye pia alikuwa amepandishwa kutoka ya vijana akadaka na mechi ikaisha kwa sare ya 0-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AISHI MANULA AMWAGIA PONGEZI ALLY SALIM KWA KAZ YA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top