• HABARI MPYA

  Thursday, April 27, 2023

  MAZOEZI YA MWISHO SIMBA SC KABLA YA OPERESHENI CASABLANCA KESHO


  WACHEZAJI wa Simba wakiwa mazoezini leo Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco kujiandaa na mchezo wa marudiano Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mabingwa watetezi, Wydad AC kesho.
  Mechi ya kwanza Simba ilishinda 1-0, bao la mshambuliaji Mkongo Jean Othos Baleke Jumamosi ya wiki iliyopita Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya CR Belouizdad ya Algeria na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zinazorudiana Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria. Mechi ya kwanza Mamelodi ilishinda 4-1 Uwanja wa Nelson Mandela mjini Baraki, Algiers, Algeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZOEZI YA MWISHO SIMBA SC KABLA YA OPERESHENI CASABLANCA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top