• HABARI MPYA

    Tuesday, April 18, 2023

    SIMBA SC WAZAWADIWA SH MILIONI 100 KABLA YA KUIVAA WYDAD JUMAMOSI


    WAKATI wachezaji wa Simba wameanza mazoezi kwa ajili ya mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Club Athletic ya Morocco, wadhamini wakuu wa timu hiyo, kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania imekabidhi bonsai ya Sh milioni 100.
    Wachezaji wa Simba walikuwa kwenye likizo fupi baada ya kibarua kigumu dhidi ya wapinzani wao, Young Africans (Yanga) katika mchezo wa ligi kuu ya NBC na kushinda kwa mabao 2-0.
    Baada ya kibarua hicho kigumu wababe hao wa Mtaa wa Msimbazi watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Wydad Club Athletic kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 10 jioni.
    Akizungumza  wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi alisema kuwa wamefuraishwa na hatua ya klabu hiyo waliyofikia katika mashindano hayo na kuamua kuongeza morarli kwa wachezaji.
    Mushi alisema kuwa wanajivunia mafanikio waliyofikia klabu hiyo na wanaamini wataendelea kung’ara katika mashindano hayo.
    Alieleza kuwa fedha hizo ni sehemu ya wajibu wao wa udhamini na wataendelea kuwapa bonasi kadri wanavyoendelea kufanya vizuri zaidi.
    “Tunajivunia sana kwa mafanikio ya klabu katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.  Huu ni mwendelezo wa kufanya vyema kwani msimu uliopita walifanya vizuri pia katika mashindano ya Kombe la Shirikisho na kufikia hatua ya robo fainali,” alisema Mushi.
    Kwa upande wake,  Afisa Mtendaji Mkuu wa klbau ya Simba, Imani Kajula alisema wapo tayari kukabiliana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo na kuwataka mashabiki wa soka kuhudhuria pambano hilo.
    Kajula alisema bonusi ya M-Bet  imeongeza morali kabla ya pambano hilo na wachezaji waliahidi kutowaangusha.
    "Sisi ni klabu yenye heshima barani Afrika na tutaendelea kufanya vyema zaidi na kuwa moja ya  klabu kubwa katika bara letu. Mara zote tunaangalia vitu vikubwa katika na tunaamini tiutafikia malengo yetu," alisema Kajula.
    Katika hatua nyingine, wachezaji wa Simba wameanza maandalizi kuelekea mchezo wa Jumamosi.
    Ofisa Habari wa Simba Ahmed Ally alisema kuwa wachezaji wawili, Sadio Kanoute na kipa chaguo la kwanza Aishi Manula ni miongoni mwa wachezaji waliojiunga na timu hiyo baada ya kuwa nje kutokana na majeraha.
    Ally alisema wawili hao watachunguzwa afya zaoi kabla ya hatua nyingine.


    Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (katikati) akizungumza wakati wa halfa maalum ya kukabisdhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh100 milioni kwa klabu ya simba baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika. Kushoto ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba,  Imani Kajula (kushoto). Kulia ni Msemaji wa klabu ya Simba, Ahmed Ally.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAZAWADIWA SH MILIONI 100 KABLA YA KUIVAA WYDAD JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top