• HABARI MPYA

  Saturday, April 22, 2023

  AZAM FC YAITANDIKA RUVU SHOOTING 3-1 MOROGORO


  WENYEJI, Ruvu Shooting wametandikwa mabao 3-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Abdul Suleiman Sopu dakika ya 41 na Ayoub Lyanga, mawili dakika ya 67 na 75, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Michael Aidan dakika ya 80.
  Azam FC inafikisha pointi 53 katika mchezo wa 27 na kusogea nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Singida Big Stars ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati Ruvu Shooting inaendelea kushika mkia na pointi zake 20 za mechi 27 pia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAITANDIKA RUVU SHOOTING 3-1 MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top