• HABARI MPYA

    Friday, April 21, 2023

    MICHEZO YA MEI MOSI YAZINDULIWA RASMI MKOANI MOROGORO


    TIMU ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Micchezo ni miongoni timu zinazoshiriki mashindano ya michezo ya Mei Mosi 2023 yanayofanyika mkoani Morogoro ambayo yamezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa. 
    Akizindua michezo hiyo amewahimiza wanamichezo kutambua kuwa michezo ni muhimu katika kuimarisha afya za wafanyakazi mahala pa kazi ili waendelee kutoa huduma bora kwa wananchi na kuongeza tija kazini.
    Mkuu huyo wa Mkoa amesema hayo Apili 20, 2023 wakati akizundua rasmi Michezo ya Kombe la Mei Mosi inayoendelea katika viwanja mbalimbali Manispaa ya Morogoro kwa kuwahusisha wafanyakazi wa umma na sekta binafsi. 
    “Mfanyakazi asiye na afya bora na legelege kwakweli hataweza kutoa huduma bora na kuzalisha kwa tija kwa kuwa mwili wake umekosa mazoezi, michezo mahala pa kazi husaidia kujenga afya na mahusiano mema miongoni mwa wafanyakazi” amesema Mkuu wa Mkoa.
    Akinukuu Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa ya mwaka 1995, Mkuu wa Mkoa Mhe. Mwasa amesema sera hiyo inasisistiza katika taifa linaloshiriki michezo ili kujenga uhusiano, uelewanona mshikamano wa kitaifa kupitia michezo mbalimbali na kuhimiza kuwa michezo siyo suala la hiyari, bali ni takwa la kisheria katika kukuza uchumi na kuboresha afya za wananchi.
    Ameahimiza vyama vya wafanyakazi na waajiri kulipa kipaumbele suala la kufanya michezo mahala pa kazi na kuweka msukumo na kuruhusu michezo mahala pa kazi.
    Aidha, amewakumbusha viongozi kutenga bajeti kwa ajili ya michezo na kutenga muda kwa wafanyakazi wao kufanya michezo ili wafanyakazi wawe na utimamu na umadhubuti wa mwili na kuongeza tija kazini.
    Maesema kuwa kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “Miaka Miwili ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Imeimarisha Michezo na Kuongeza Ufanisi Kazini, Kazi Iendelee” na kusema kuwa ni ukweli usiopingika mwanamichezo kasi yake ya kufanyakazi ni nzuri na kusisitiza kuwa wafanyakazi wameelewa dhana ya michezo na kugundua kuwa michezo inaimarisha afya na kuuweka mwili imara na matokeo yake kupunguza kasi ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wafanyakazi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHEZO YA MEI MOSI YAZINDULIWA RASMI MKOANI MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top