• HABARI MPYA

  Saturday, April 22, 2023

  KITAYOSCE YAICHAPA JKT 3-2 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUPANDA


  WENYEJI, Kitayosce wamefufua matumaini ya kupanda Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya JKT Tanzania leo katika mchezo wa Championship Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Mechi nyingine za Championship leo, Mbuni FC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Pamba SC, Transit Camp imeichapa Mbeya Kwanza 1-0 na Fountain Gate imetoka sare ya 1-1 na Mashujaa FC.
  Sasa msimamo wa Championship ni JKT Tanzania inaendelea kuongoza kwa pointi zake 62 za mechi 26 ikiwa imekwishajihakikishia kupanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya Pamba kutoa sare.
  JKT inafuatiwa na Kitayosce ponti 53 na Pamba FC 52 baada ya wote kucheza mechi 25 na mojawapo itapanda Ligi Kuu pia ikimaliza nafasi ya pili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KITAYOSCE YAICHAPA JKT 3-2 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUPANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top