• HABARI MPYA

  Sunday, April 16, 2023

  SIMBA SC YACHAPA YANGA 2-0 INONGA NA KIBU


  WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mtani, Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na beki Mkongo, Inonga Baka ‘Varane’ dakika ya pili na kiungo Kibu Dennis Prosper dakika ya 32.
  Kwa ushindi huo, Simba SC imefikisha pointi 63, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YACHAPA YANGA 2-0 INONGA NA KIBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top