• HABARI MPYA

  Friday, April 28, 2023

  RAIS SAMIA SASA KUZAWADIA SH MILIONI 10 KILA BAO SIMBA NA YANGA CAF


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amepandisha dau la zawadi kwa mabao yanayofungwa na klabu za Simba na Yanga kwenye michuano ya Afrika kutoka Sh. Milioni 5 hadi Milioni 10 kwa kila bao zikifuzu hatua ya nusu fainali.
  Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema mabao yatakayolipiwa Sh. Milioni 10 ni yale ambayo yatafungwa ama katika dakika 90 au 30 za nuongeza, na si yatakayopatikana kwa mikwaju ya penalti ya baada ya dakika 120 za mchezo.
  Pamoja na hayo, Rais Samia amezitakia kila la kheri Simba na Yanga katika mechi za marudiano za Robo Fainali ya michuano ya klabu leo na Jumapili.
  Simba watamenyana na wenyeji, Wydad Athletic Club leo katika mchezo wa marudiano Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco kujiandaa.
  Mechi ya kwanza Simba ilishinda 1-0, bao la mshambuliaji Mkongo Jean Othos Baleke Jumamosi ya wiki iliyopita Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya CR Belouizdad ya Algeria na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zinazorudiana Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria. Mechi ya kwanza Mamelodi ilishinda 4-1 Uwanja wa Nelson Mandela mjini Baraki, Algiers, Algeria.
  Kwa upande wao Yanga Jumapili watamenyana na Rivers United ya Nigeria katika mchezo wa marudiano Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mechi ya kwanza Yanga ilishinda 2-0, mabao ya mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele Uwanja wa Venue Godswill Akpabio International mjini Uyo, Nigeria Jumapili iliyopita.
  Ikumbukwe mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambazo mechi ya kwanza zilitoka sare ya 1-1 Misri Jumapili iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS SAMIA SASA KUZAWADIA SH MILIONI 10 KILA BAO SIMBA NA YANGA CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top