• HABARI MPYA

  Saturday, April 22, 2023

  ARSENAL YAPIGANIA SARE 3-3 NA VIBONDE SOUTHAMPTON EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal walipambana na kupata sare ya 3-3 na Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Ijumaa Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Southampton yalifungwa na Carlos Alcaraz dakika ya kwanza, Theo Walcott dakika ya 14 na Duje Caleta-Car dakika ya 66, wakati ya Arsenal yalifungwa na Gabriel Martinelli dakika ya 20, Martin Odegaard dakika ya 88 na Bukayo Saka dakika ya 90.
  Kwa matokeo hayo, Arsenal inafikisha pointi 75 katika mchezo wa 32 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao, Southampton wanafikisha pointi 24 katika mchezo wa 32 pia ingawa wanaendelea kushika mkia katika Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPIGANIA SARE 3-3 NA VIBONDE SOUTHAMPTON EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top