• HABARI MPYA

  Tuesday, April 25, 2023

  MAAFISA MICHEZO WAAGIZWA KUANDAA KAZI DATA YA WANAMICHEZO KATIKA MAENEO YAO


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana @pindi.chana amewaagiza Maafisa Michezo kote nchini waandae Kanzi Data ya Wanamichezo katika maeneo yao ili kupata takwimu za wanaojihusisha na sekta hiyo.
  Mhe. Balozi Pindi Chana ametoa agizo hilo Aprili 23, 2023 jijini Dodoma wakati wa Pambano la Ngumi la Hisani Kwa ajili ya kuchangia Fedha za kununua taulo za kike lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma akitoa wito kwa Wawekezaji wajitokeze kuwekeza katika Sekta hiyo.
  "Natoa wito kwa Shirikisho la Ngumi nchini, lisimamie taratibu za mchezo huu kulinda maslahi ya Wana masumbwi pamoja na kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi kushiriki mchezo huu" Amesisitiza Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana.
  Aidha, ametoa wito kwa jamii ilinde na kuhifadhi Mila na Desturi zilizo njema na zinazokubalika hapa nchini akikemea vikali tabia za mapenzi na ndoa za jinsia moja kwamba hazina nafasi katika Taifa la Tanzania.
  Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa pambano hilo amesema ni fursa katika Mkoa wa Dodoma ikiwemo kutangaza vivutio vya Mkoa huo ikiwemo Kondoa Irangi, Mkunguneo na Kolo.
  Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Lady in Red Promotion Mhe. Sophia Mwakagenda amesema pambano hilo lina lengo la kupata fedha kwa ajili ya kuwanunulia watoto wa kike taulo ili kuwawezesha kuhudhuria masomo yao kwa umakini zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAAFISA MICHEZO WAAGIZWA KUANDAA KAZI DATA YA WANAMICHEZO KATIKA MAENEO YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top