• HABARI MPYA

  Thursday, April 27, 2023

  DE BRUYNE APIGA MBILI MAN CITY YAITANDIKA ARSENAL 4-1


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameweka hai matumaini ya kutwaa tena ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu baada ya kuitandika Arsenal mabao 4-1 usiku wa Jumatano Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne mawili, dakika ya saba na 54, beki wa England John Stones dakika ya 45 na mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland dakika ya 90 na ushei, wakati la Arsenal limefungwa na beki mwingine wa England, Robert Holding dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 73 katika mchezo wa 31, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakiziwa pointi mbili na Arsenal inayoendelea kuongoza Ligi ikiwa imecheza mechi mbili zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE BRUYNE APIGA MBILI MAN CITY YAITANDIKA ARSENAL 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top