• HABARI MPYA

  Monday, April 24, 2023

  PRISONS WAICHAPA GEITA GOLD 3-1 NYANKUMBU


  TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Jeremiah Juma dakika ya tatu, Samson Mbangula dakika ya 68 na Edwin Barua dakika ya 75, wakati la Geita Gold limefungwa na Juma Luizio dakika ya 83.
  Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 31 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake  37 nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 27.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS WAICHAPA GEITA GOLD 3-1 NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top