• HABARI MPYA

  Thursday, August 04, 2022

  SIMBA YAMTAMBULISHA KIUNGO MNIGERIA NELSON OKWA


  KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo Mnigeria, Nelson Esor-Bulunwo Okwa (28) kuwa mchezaji wake mpya wa saba kuelekea msimu ujao.
  Okwa anayetokea klabu ya Rivers United ya kwao anakuwa mgeni mpya wa tano baada ya beki Muivory Coast, Mohamed Outtara kutoka El Hilal ya Sudan, kiungo Mnigeria, Victor Akpan kutoka Coastal Union, winga Mghana, Augustine Okrah kutoka klabu ya Asante Kotoko ya kwao na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao pia.
  Wengine ni wazawa, beki Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar ya Bukoba na mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza ya Mbeya iliyoshuka Daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMTAMBULISHA KIUNGO MNIGERIA NELSON OKWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top