• HABARI MPYA

  Sunday, August 21, 2022

  WABRAZIL WAENDELEA KUING’ARISHA SINGIDA STARS LIGI KUU


  WENYEJI, Singida Big Stars wamepata ushindi wa pili mfululizo nyumbani katika mechi mbili za awali za Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo pia kuilaza Mbeya City 2-1 Uwanja wa LITI, zamani Namfua, Singida.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi, kwani Big Stars walilazimika kutoka nyuma baada ya Mbeya City kutangulia na bao la Sixtus Sabilo dakika ya 50.
  Walikuwa wachezaji wapya watatu kutoka Brazil walioipa Singida ushindi huo, Dario Federico akifunga bao la kwanza dakika ya 53 kwa penalti baada ya na Bruno Gomez akafunga la ushindi dakika ya 61 akimalizia pasi ya ‘nduguye’ Peterson Cruz.
  Singida Stars wanafikisha pointi sita baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Tanzania Prisons hapo hapo LITI bao la tik tak la Mbrazil Peterson Cruz.
  Mbeya City wao wanapoteza mechi ya kwanza baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji hapo hapo LITI.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WABRAZIL WAENDELEA KUING’ARISHA SINGIDA STARS LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top