WENYEJI. Simba SC wameanza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Geita Gold usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na winga Mghana, Augustine Okrah dakika ya 37 na Wazambia, mshambuliaji, Moses Phiri dakika ya 61 na kiungo Clatous Chama kwa penalti dakika ya 81.
Ushindi ni sawa na kupoza maumivu kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kuchapwa 2-1 na watani, Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii Jumamosi hapo hapo Mkapa.
0 comments:
Post a Comment