• HABARI MPYA

  Sunday, August 07, 2022

  SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI KUTOKA SERBIA


  KLABU ya Simba imemtambulisha mshambuliaji Mserbia, Dejan Georgijević kuwa mchezaji wake mpya wa nane kuelekea msimu ujao.
  Wengine wapya ni beki Muivory Coast, Mohamed Outtara kutoka El Hilal ya Sudan, viungo Wanigeria, Victor Akpan kutoka Coastal Union, Nelson Esor-Bulunwo Okwa kutoka Rivers United ya kwao, winga Mghana, Augustine Okrah kutoka klabu ya Asante Kotoko ya kwao na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco ya kwao pia.
  Wengine ni wazawa, beki Nassoro Kapama kutoka Kagera Sugar ya Bukoba na mshambuliaji Habib Kyombo kutoka Mbeya Kwanza ya Mbeya iliyoshuka Daraja.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI KUTOKA SERBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top