• HABARI MPYA

  Tuesday, August 16, 2022

  RASMI, SAMATTA AREJEA KRC GENK YA UBELGIJI


  RASMI, klabu ya KRC Genk imetangaza kumrejesha mshambuliaji wake wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta.
  Nahodha huyo wa Taifa Stars alianzia maisha yake ya soka ya Ulaya katika nchini Ubelgiji katika KRC Genk mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kuhamia Aston Villa ya England mwaka 2020.
  Alicheza Villa nusu msimu kabla ya kwenda Fenerbahce ya Uturuki kwa mkopo, ambako mwishoni mwa msimu alinunuliwa moja kwa moja.
  Alicheza Fenerbahce hadi kwa muda mfupi kabla ya kutolewa kwa mkopo Royal Antwerp ya Ubelgiji hadi mwishoni mwa msimu uliopita na sasa anarejea Genk.
  Kisoka, Samatta mwenye umri wa miaka 29 aliibukia African Lyon mwaka 2008, kabla ya kwenda Simba SC mwaka 2010 ambayo ilimuuza Mazembe mwaka 2011.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASMI, SAMATTA AREJEA KRC GENK YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top