• HABARI MPYA

  Tuesday, August 09, 2022

  YANGA KUANZIA SUDAN KUSINI, SIMBA MALAWI LIGI YA MABINGWA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wataanzia ugenini dhidi ya Zalan ya Sudan Kusini katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati watani wao, Simba wataanzia ugenini pia dhidi ya Big Bullets ya Malawi.
  Mshindi kati ya Yanga na Zalan atakutana na mshindi kati ya St. George ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan, wakati mshindi kati ya Simba na Big Bullets atamenyana na mshindi kati ya Red Arrows ya Zambia na Primiero do Agosto ya Angola.
  Mechi za kwanza za Raundi ya kwanza zitachezwa kati ya Septemba 9 na 11 na marudiano Septembe 16 na 18, wakati za Raundi ya pili zitafuatia kati ya Oktoba 7 na 9 na marudiano Oktoba 14 na 16.
  Washindi wa Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa watafuzu hatua ya makundi na watakaotolewa hatua wataangukia kwenye kapu la kuwania kucheza Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUANZIA SUDAN KUSINI, SIMBA MALAWI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top