• HABARI MPYA

  Thursday, August 04, 2022

  SINGIDA STARS YAICHAPA ZANACO YA ZAMBIA 1-0 LITI


  BAO pekee la Deus Kaseke dakika ya 14 limeipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki kuhitimisha tamasha la Singida Big Day leo Uwanja wa LITI, zamani Namfua mjini Singida. 
  Mchezo huo ulitanguliwa na shamrashamra mbalimbali, burudani ya muziki kutoka kwa msanii Harmonize kabla ya kutambulishwa kikosi kamili cha timu hiyo kwa ajili ya Ligi Kuu, kikiwa kimesheheni wachezaji kadhaa maarufu waliowika Simba na Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA STARS YAICHAPA ZANACO YA ZAMBIA 1-0 LITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top