• HABARI MPYA

    Tuesday, August 23, 2022

    KINDA WA AZAM, TEPSIE EVANS AONGEZWA TAIFA STARS


    KOCHA Mdenmark, Kim Poulsen amemuongeza kiungo Tepsi Evans wa Azam FC kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Uganda Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
    Timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe na mshindi atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KINDA WA AZAM, TEPSIE EVANS AONGEZWA TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top