• HABARI MPYA

  Sunday, August 28, 2022

  TAIFA STARS MGUU NJE CHAN, YACHAPWA 1-0 NA UGANDA DAR


  TANZANIA imejiweka kwenye nafasi ngumu ya kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuchapwa 1-0 na Uganda jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la The Cranes lililoizamisha Taifa Stars leo limefungwa na Travis Mutyaba dakika ya 87 na sasa timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe na mshindi atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS MGUU NJE CHAN, YACHAPWA 1-0 NA UGANDA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top