• HABARI MPYA

  Sunday, August 21, 2022

  MATHEO APIGA MBILI KMC 2-2 NA POLISI

   

  TIMU ya Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya 2-2 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Mabao ya Polisi Tanzania yamefungwa na Ally Salim Kipemba dakika ya pili na Chilo Mkama dakika ya 10, wakati ya KMC yote yamefungwa na Matheo Anthony Simon dakika ya tano na 47.
  Timu zote zimeokota pointi ya kwanza leo baada ya wote kupoteza mechi zao za awali, KMC ilifungwa 1-0 na Coastal Union na Polisi ikichapwa 2-1 na Yanga hapo hapo Sheikh Amri Abeid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MATHEO APIGA MBILI KMC 2-2 NA POLISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top