• HABARI MPYA

  Saturday, August 20, 2022

  DEJAN APIGA LA PILI SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0


  VIGOGO, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Kagera Sugar ya Bukoba mabao 2-0 usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa washambuliaji wake wapya, Mzambia Moses Phiri dakika ya 42 na Mserbia Dejan Geirgejevic dakika ya 81.
  Ni ushindi wa pili kwa Simba SC baada ya awali kuichapa Geita Gold 3-0 na kipigo cha pili kwa Kagera Sugar kufuatia kufungwa 2-1 na Azam kwenye mechi za kwanza zote zikichezwa Dar es Salaam.
  Mzambia, Moses Phiri leo amefunga bao lake la pili baada ya kufunga pia kwenye mechi na Geita Gold, wakati Dejan ndio anafungua akaunti yake ya mabao Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DEJAN APIGA LA PILI SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top